Enter your keyword

post

HOT TOPIC: Binadamu walianza lini kuongea, na kwa nini?

Watu wa kale walianza kujifunza lini kuzungumza? Je, inawezekana kufahamu asili ya maelfu ya lugha zinazozungumzwa leo kutoka kwa mtu mmoja wa kale?

Mwandishi na mtaalamu wa lugha Michael Rosen anatafiti. Binaadamu ni viumbe ambao wana lugha, kitu kinachotufanya kuwa wa kipekee miongoni mwa wanyama wote, ” anasema Maggie Tallerman, Profesa wa masuala ya lugha katika chuo cha Newcastle. Uwezo huu wa kuwasiliana unaonekana kama moja ya mabadiliko makubwa, kuliko mengine yeyote, na kwa sababu hii, watu wamekuwa na shauku ya kufahamu asili za lugha. ‘Lugha ni moja kati ya vitu vinavyotufanya kuwa binaadamu, ” anasema Robert Foley, mwana anthropologia na profesa wa stadi za historia ya binaadamu katika Chuo cha Cambridge.

Kuna lugha zaidi ya 6,500 duniani siku hizi, lakini ni kwa namna gani wana sayansi watafahamu lugha ya kwanza kuliko zote? Ikiwa tutaulizwa kuhusu kutaja ”lugha ya kale”, tunaweza kufikiri kuwa ni ya Babylon,Sanskrit au ya wamisri wa kale. Profesa Tallerman anasema lugha nyingi tunazoziita kuwa za kale hazina zaidi ya umri wa miaka 6,000, umri sawa na lugha nyingine zozote zinazozungumzwa siku hizi. Chanzo cha lugha kinaweza kuwa miaka takriban 50,000 iliyopita, na wataalamu wengi wa lugha wanafikiri ni miaka mingi zaidi nyuma. ”Wengi wetu tunaamini tunaweza kurudi nyuma miaka nusu milioni iliyopita anasema Profesa Tallerman.

Ingawa kuna utajiri wa lugha mbalimbali , ”inawezekana kuwa lugha zetu za sasa zinatokana na lugha za watu wa kale,”anasema profesa Foley. Ingawa kunaweza kuwa na lugha nyingine nje ya vizazi vilivyotangulia, lugha tunazoziona sasa pengine zinatoka kwenye lugha hiyo hiyo. Mabaki ya watu wetu wa kale, yanatupa viashiria vichache kufahamu lini tulianza kuzungumza. ”kuzungumza, kwa namna nyingine ni kupumua, ” anasema Profesa Foley, ”tunapumua tukitoa sauti mbalimbali.” Ili kuweza kufanya hivyo, tunahitajika kuwa na uwezo wa kudhibiti misuli yetu zaidi ya miili yetu kama ”mapafu yetu yaliyojengeka na yenye neva nyingi zinazokwenda.

Neva hizi zote zinamaana kuwa ”uti wetu wa mgongo ni mwembamba kiasi kwenye eneo hilo Julio ya sokwe, na mifupa yake inapaswa kuwa mipana pia.” Ukitazama viumbe wa kale walioishi miaka takribani 600,000 iliyopita, wana eneo la uti wa mgongo lililotanuka. Hii inatupa viashiria kufahamu ni lini mwanadamu alianza kutumia lugha. Mbali na rekodi kuhusu mabaki ya watu wa kale,stadi za jenetiki pia zinatoa ishara namna ya kufahamu lugha ilianza lini. Kuna jeni ziitwazo FOXP2, ambazo ziko kwa viumbe vyote,”anasema prof Foley, ”lakini sisi binadamu tunazo kwa kiasi kidogo”. Mabadiliko ya jeni hii ”yanaweza kusaidia kueleza kwa nini binadamu wanaweza kuzungumza na solte hawawezi.Tunajua ushahidi huu ni muhimu kwenye maendeleo ya lugha na mazungumzo.

Je ubongo wa watu wa zamani husaidia kujua lugha ilianza lini? Hapana. Kwa sababu ndogo tu kuwa hatujui ukubwa gani wa ubongohusaidia kuunda lugha.”Ukweli ni kuwa viumbe sokwe ubongo wao ni mkubwa kuliko wa binadamu kwa kuwa walikuwa wanyama wakubwa,”anasema Prof Tallerman, mtafiti.

Source: BBC News

No Comments

Add your review

Your email address will not be published.