Enter your keyword

post

Wanafunzi 20 wa Afrika Kusini walitengeneza ndege ‘nyumbani’ kwa safari ya Cape mpaka Cairo

Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi nchini Afrika Kusini ipo njiani katika safari ya kutoka jiji la Cape Town kuelekea Cairo. Tayari ndege hiyo imeshatua salama katika kitoa chake cah kwanza nchini Namibia.

Inatarajiwa safari hiyo ya kutoka mji wa kusini wa Cape Town mpaka nchini Misri sawa na umabli wa kilomita 12,000 itachukua muda wa wiki sita kukamilika.

Ndege hiyo yenye viti vine aina ya Sling 4 iliundwa na kundi la wanafunzi 20 waliochini ya umri wa miaka 20 kutoka katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo. “Lengo la kampeni yetu hii ni kulionesha bara la Afrika kuwa chochote kinawezekana iwapo utawekeza akili yako katika jambo hilo,” ameeleza moja ya marubani, Megan Werner, ambaye ni msichana wa miaka 17.

Wanafunzi hao waliitengeneza ndege hiyo katika kipindi cha wiki tatu, wakiunganisha vifaa vilivyonunulia kwenye kampuni moja nchini Afrika Kusini.

“Nikiiangalia hii ndege, huwa ninaona fahari ya hali ya juu kwa kile nilichokifanya. Siamini kile tulichokifanya. Ninaiona kama mtoto wangu. Ninamtukuza mtoto (ndege),” ameeleza Agnes Keamogetswe Seemela, msichana kutoka katika jimbo la Gauteng mwenye umri wa miaka 15.

“Inapaa uzuri kabisa, na ukiwa juu, mwonekano wa chini ni mzuri kweli,” ameeleza kulingana na safari ya kwanza ya ndege hiyo kutoka jiji la Johannesburg mpaka Cape Town, kabla ya kuanza safari ya Misri.

“Nilishiriki katika kuunda eneo la kti la ndege hiyo pamoja na mabawa yake.”

Msichana huyo mdogo anaamini juhudi zake zitachangia kuchochea wasichana wenzake.

“Awali watu wa jamii yangu walishtushwa sana – hwakuamini nilipowaambia kuwa nimeshiriki kuunda ndege itakayopaa Cape Town mpakaCairo,” amesema.

“Lakini kwa sasa, wote wanajivunia mimi.”

Megan, 17, ndiye alianzisha mpango huo unaofahamika kama U-Dream Global ambao ulipokea maombi kutoka kwa zaidi ya wanafunzi 1,000.

Yeye pamoja na wenzake sita kutoka kwenye mpango huo walipata leseni ya urubani. Ni hao wanafunzi sita ndio watakaopokeza kuendesha ndege hiyo.

“Kupata leseni ya urubani ni sawa na kumaliza shahada – kufanya hivyo wakati ambapo nilitakiwa nijisomee kwaajili ya mitihani yangu ya shule haikuwa jambo rahisi,” amesema Megan, ambaye alifanya mitihani ya kumaliza shule mwezi Oktoba 2018, kipindi hiko pia akijiandaa na mafunzo yake ya urubani.

Baba wa msichana huyo, Des Werner, ni rubani wa ndege za abiria, na anasema kuwa kuunda ndege hiyo kunahitaji walau saa 3,000 za kazi (sawa na siku 125).

“Ukigawanya muda huo kwa watoto 20 walio chini ya uangalizi unaweza kuikamilisha ndani ya wiki tatu. Injini na vifaa vya mawasiliano viliwekwa na wataalamu, lakini muundo wote ulifanywa na watoto,” amesema.

Kitua cha kwanza cha safari hiyo ni mji wa kusini katika pwani ya Namibia wa Luderitz, na tayari wameshatua huko.

Ndege hiyo ina uwezo wa kupaa angani kwa muda wa saa sita na nusu, na itakuwa na vituo kadhaa katika nchi za Zimbabwe, Malawi, Tanzania, Kenya, Ethipia na Eritrea kabla ya kufika Misri.

Katika safari ya kurudi, watatumia njia tofauti na watasimama katika nchi za Uganda, Rwanda, Zambia na Botswana.

Kutakuwa na ndege nyengine aina ya Sling 4 pkwa ajili ya usaidizi.

Marubani hao wanafunzi wanapanga kuzungumza na wanafunzi wenzao katika nchi zote ambazo watasimama.

“Ni kitu kizuri kuona ni kwa namna gani watu wanavutia na kushawishika na kile ambacho tumefanya,” amesema rubani Megan.

Source: BBC News

 

 

 

 

 

 

No Comments

Add your review

Your email address will not be published.